Friday, 3 October 2014

UJASIRIAMALI KURAHISISHA MAISHA.....ARUSHA

                  Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Adson Kagiye Mayagila                   akiwasilisha mada katika semina ya Ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo mapema hii                      leo.Picha na Mariam Hizza.

   Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mafunzo   ya semina ya Ujasiriamali katika ukumbi wa chuo hicho hii leo.Picha na Mariam Hizza.

Wakufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha ambao pia walikuwa ndio wawasilishaji wa mada za semina ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja.Wa tatu kutoka kushoto waliokaa ni Makam Mkuu wa Chuo,Elifuraha Samboto.Picha na Mariam Hizza.

Habari na Mariam Hizza,
 Wakufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {A.J.T.C} wametoa semina ya siku tatu kwa wanafunzi wake iliyomalizika mapema leo chuoni hapo.
  
Wakitoa semina hiyo baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho waliwasisitiza wanafunzi pamoja na watu wengine kujihusisha na ujasiliamali ili kuondokana na lindi la umaskini.

 Akizindua semina hiyo mkuu wa chuo hicho bwana Joseph mayagilla alitoa maada iliyowafundisha  wanafunzi ni jinsi gani wanaweza kuhifadhi pesa zao ili kufikia malengo na kuwa wajasiliamali wakubwa.
   ,, Unatakiwa ujue kuhifadhi pesa zako na uwe na uelewa ipi ni pesa mazao na ipi ni pesa mavuno 
     hii  itakusaidia kujua jinsi ya kugawanya fedha zako.Alisema bwana Mayagilla.

  Mratibu wa semina hiyo bwana Andrea Ngobole aliwaasa wajasiliamali kujiwekea misingi katika biashara zao ili kuepuka hasara zinazoepukika.

Bwana Ngobole alisema kuwa ukitaka kuwa mjasiliamali inatakiwa uzingatie maadili ya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kuwajali na kuwaheshimu wateja wako na watu wote kitu kitakachokuongezea wateja.
   ,, Ukiwa mjasiliamali unatakiwa kuwa mvumilivu pia unatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yako          na maadili kwa biashara yako mwenyewe.Alisema bwana Ngobole,,

 Licha ya kutoa semina pia ilitolewa burudani iliyofanywa na walimu pamoja na wanafunzi lengo likiwa ni kuburudisha pamoja na kuleta usikivu kwa wasikilizaji.

Makamu mkuu wa chuo hicho bwana Elifuraha Samboto alihitimisha kwa kuwashukuru wote waliohudhuria semina hiyo pamoja na kuwasihi wawe na tabia ya kujisomea vitabu na kuhudhuria semina ilikuongeza ujuzi na kujua changamoto wanazopata wajasiliamali wakubwa na jinsi ya kukabiliana nazo.
  

Wednesday, 1 October 2014

Semina ya ujasiliamali ndani ya chuo cha uandishi wa habari Arusha ya toa fursa.

Na.ELIZABETH SAID ADYSWELE

Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Akifungua semina ya ujasiriamali mapema leo. NA ELIZABETH SAID
















Mkurugenzi wa chuo chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha bwana Joseph Mayagila amefungua semina ya siku tatu ya ujasiriamali leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
Bwana Joseph Mayagila amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya ujasiriamali.
Alisema kuwa ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima ajue kupanda mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya kupanda mbegu.
“Unaweza kuhangaika sana kwa lengo  la kupata fedha mbegu, kwa kuwa mbegu hizo zitazalisha fedha nyingi zaidi kupitia mbegu hiyo”
Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni hapo ikiwemo kozi ya uandishi wa  habari, ualimu,sekretari pamoja na kozi ya kompyuta.
Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya mikakati ya kibiashara,  na mada ya huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo bw, Adrea Ngobole.  
Bwana Maygila alisema kuna kuuuza na kununua lakini sio kila mtu anaweza kuuza na kuwataka wote kujenga fikra zao katika kuuza ila waweze kujenga maisha yao
Alisema kama mtu anataka kufanikiwa maishani na kutaka kununua vitu vya thamani ni lazima mtu ajipange vizuri katika  kuuza
“Duniani kuna kuuza na kununua huwezi kukwepa kununua lakini  sio kila mtu anaweza kuuza, unaweza kuuza mawazo, jambo na bidhaa” Alisema Mayagila
Mayagila aliwashauri wanafunzi wake kujiunga   kwenye taasisi za kifedha kwani mkopo ni fedha mbegu na zitawasaidia  kufanikisha biashara zao na kuzaa zaidi
Amehitimisha ufunguzi wa  semina hiyo kwa kusema kwamba ili mtu yeyote afanikiwe ni lazima kusoma vitabu mbalimbali 
“Nyumba isiyyo na vitabu ni mfu, akili isiyopenda kusoma ni mfu pia ,ili uweze kufanikiwa nilazima ulipe gharama za kufanikiwa”
Na baada ya uzinduzi huo semina ilianza rasmi  ambapo Bw. Onesmo Mbise alifundisha maada ya Bussiness Planing na kuzungumuzia zaidi mikakati mahususi kuhusu biashara

                           Bw. Onesmo Elia Mbise, Akitoa mada

        

 Mkufunzi wa pili Bw. Christian Ndege yeye alifundisha somo la Customer Care na kueleza mbinu mbalimbali za kuvutia wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri , kumheshimu na kumtambua kuwa ni bosi na kumwomba radhi pale tu unapomkosea
Nae kwa upande wake Bw. Andrea Ngobole aliwasilisha somo la tatu kwa siku ya leo kuhusu misingi/miongozo ya mjasiriamali Bw. Ngobore amesema mjasiriamali yeyote ni vyema kuwa na marafiki  wajasiriamali ili kufanikiwa kupata taarifa mbalimbali kuhusu Biashara

                                  Bw. Andrea Ngobole Akiwasilisha maada                                                                    

Wakati huo huo pia ametaja mambo ambayo mjasiriamali anapaswa kuyaepuka  ikiwa ni pamoja na kulaumu, starehe, kuamini uchawi, umbea na mengine mengi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kufika mbali na kufanikiwa kibiashara


Baadhi ya wanafunzi wa kiwa katika semina chuoni hapo

Aidha wanafunzi walio wengi chuoni hapo wameipoke kwa furaha semina hiyo ambayo
            itaendelea tena mapema kesho asubuhi saa 3 kamili