Friday, 3 October 2014

UJASIRIAMALI KURAHISISHA MAISHA.....ARUSHA

                  Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Adson Kagiye Mayagila                   akiwasilisha mada katika semina ya Ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo mapema hii                      leo.Picha na Mariam Hizza.

   Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mafunzo   ya semina ya Ujasiriamali katika ukumbi wa chuo hicho hii leo.Picha na Mariam Hizza.

Wakufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha ambao pia walikuwa ndio wawasilishaji wa mada za semina ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja.Wa tatu kutoka kushoto waliokaa ni Makam Mkuu wa Chuo,Elifuraha Samboto.Picha na Mariam Hizza.

Habari na Mariam Hizza,
 Wakufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {A.J.T.C} wametoa semina ya siku tatu kwa wanafunzi wake iliyomalizika mapema leo chuoni hapo.
  
Wakitoa semina hiyo baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho waliwasisitiza wanafunzi pamoja na watu wengine kujihusisha na ujasiliamali ili kuondokana na lindi la umaskini.

 Akizindua semina hiyo mkuu wa chuo hicho bwana Joseph mayagilla alitoa maada iliyowafundisha  wanafunzi ni jinsi gani wanaweza kuhifadhi pesa zao ili kufikia malengo na kuwa wajasiliamali wakubwa.
   ,, Unatakiwa ujue kuhifadhi pesa zako na uwe na uelewa ipi ni pesa mazao na ipi ni pesa mavuno 
     hii  itakusaidia kujua jinsi ya kugawanya fedha zako.Alisema bwana Mayagilla.

  Mratibu wa semina hiyo bwana Andrea Ngobole aliwaasa wajasiliamali kujiwekea misingi katika biashara zao ili kuepuka hasara zinazoepukika.

Bwana Ngobole alisema kuwa ukitaka kuwa mjasiliamali inatakiwa uzingatie maadili ya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kuwajali na kuwaheshimu wateja wako na watu wote kitu kitakachokuongezea wateja.
   ,, Ukiwa mjasiliamali unatakiwa kuwa mvumilivu pia unatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yako          na maadili kwa biashara yako mwenyewe.Alisema bwana Ngobole,,

 Licha ya kutoa semina pia ilitolewa burudani iliyofanywa na walimu pamoja na wanafunzi lengo likiwa ni kuburudisha pamoja na kuleta usikivu kwa wasikilizaji.

Makamu mkuu wa chuo hicho bwana Elifuraha Samboto alihitimisha kwa kuwashukuru wote waliohudhuria semina hiyo pamoja na kuwasihi wawe na tabia ya kujisomea vitabu na kuhudhuria semina ilikuongeza ujuzi na kujua changamoto wanazopata wajasiliamali wakubwa na jinsi ya kukabiliana nazo.
  

No comments:

Post a Comment