kutoka kushoto ni muuzaji wa nyama yambuzi Bw.Rafael Isaya aakizungumza na mteja maeneo ya kwa Morombo Arusha
Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama
katika soko la kwa morombo lililopo mkoani arusha wameeleza jinsi
wanavyonufaika na kazi hiyo ya uchomaji wa nyama ya mbuzi.
Akizungumza na waandishi wahabari
mmoja wa wafanyabiashara hao Bw.Rafaeli Issaya amesema kuwa,biashara ya
uchomaji wa nyama ya mbuzi imemnufaisha kwa kiwango kikubwa cha maisha yake na
familia yake.
Amesema kuwa nyama hiyo ya mbuzi
iliyochomwa kiasi cha kilo moja huuzwa kwa bei ya shilingi elfu sita wakati
mguu uliochomwa wennye kilo mbili huuzwa kwa shilingi elfu kumi.
Pia Bw.Rafaeli amesema kuwa kwa siku
za kawaida huchinja mbuzi wawili hadi watatu lakini kwa siku za wikiendi anaweza
kuchinja mbuzi wanne mpaka mpaka sita na kuuza nyama yote.
‘’kwa siku za kawaida nachinja mbuzi
watatu lakini inapofika siku za wikieni nachinja mbuzi watano mpaka sita na
nauza nyama yote inaisha maana wateja wanakuwa wengi sehemu zote’’
Pichani ni Bw. Rafael Isaya akimuhudumia mteja
Aidha Bw John Paul ambaye pia
nimfanya biashara wa nyama choma ameeleza changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo
ya wafanya biashara hao kuwa wengi sehemu hiyo na huku wengine wakiwa na wateja
wao wa kudumu.
Amemalizia kwa kutoa ushauri kwa
wafanya biashara wengine kufanya kazi hiyo katika hali ya usafi ili kuepuka
mlipuko wa magonjwa ambayo ni hatari sana kwa binadamu.
Habari na ;OMARI SINGANO pamoja na GUDILA KULAYA
No comments:
Post a Comment