Kutuka kushoto ni mwandishi wa gazeti la ajtc akimuhoji mmiliki wa saluni iliyoko kwa morombo Arusha mama Sundy mapema leo.picha na MARIAM HIZZA.
Mteja akiwa saluni kwa mama Sundy akihudumiwa.picha na MARIAM HIZZA.
Habari na MARIAM HIZZA,
Wafanyakazi
wa saloon wamelalamikia wateja wao ambao wana tabia ya kutaka kupunguziwa bei
ambayo inakuwa ndogo ukilinganisha na maisha yalivyopanda kwa sasa.
Akizungumza jana na mwandishi wetu mmoja
wa wafanyakazi wa saloon iliyoko arusha maeneo ya kwa morombo aliyejitambulisha
kwa jina la mama Sundy alisema kuwa wateja wake wajaribu kuangalia na hali ya
maisha yalivyo.
Mama huyo alisema kuwa licha ya wateja
kutaka kupunguziwa bei pia wakikataa huwa wanahama na kuenda saloon nyingine
kitendo ambacho kinawapunguzia wateja.
“Utakuta mteja anataka apunguziwe bei na ukiangalia bei
wanayotaka ni ndogo sana ukilinganisha na maisha ya sasa yamepanda yako juu
sana”alisema mama Sundy.
Hata hivyo mama
sundi alisema inabidi wateja ifike kipindi wawe waelewa kwani hela hiyohiyo hutumika kulipia vyumba na hata kutumia kwa ajili ya mahitaji ya familia.
Wateja walisema
kuwa ni kweli kuna baadhi ya wateja wamekuwa na tabia hiyo ambayo hurudisha
nyuma maendeleo.
Mmoja wa wateja hao
aliyejitambulisha kwa jina la Halima alisema kuwa wapo baadhi ya wateja wenye
tabia hiyo na kusema kuwa wawe wanawaonea huruma kwani hali ya maisha kwa sasa
ni ngumu.
" Wateja tunatakiwa tuiheshimu kazi ya saloon na kuiona ni
kazi kama kazi nyingine tujaribu kuwaonea huruma kwani nao
wana familia zinazowategemea”alisema bi Halima.
Mama sundy
alimalizia kwa kusema ifike kipindi watu wakubali kazi za watu na kuziheshimu
kwani kufanya hivyo kutasaidia maisha kuwa mepesi hali ambayo itasaidia
kupunguza umaskini hapa nchini.
No comments:
Post a Comment