Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha kwa
kufanyakazi za ujasiriamali na kuacha kuwategemea wanaume zao katika kuendesha
maisha.
Wito huo umetolewa na wanawake wauzao chakula (mama
ntilie) jijini Arusha walipokuwa wanaongea na mwandishi wa habari hizi mapema
leo.
Baadhi ya vyombo vinavyotumiwa na wajasiriamali hao(picha na Nassor Amour) |
‘’Inatakiwa wanawake tujishughulishe tuache kumtegemea mwanaume kwa kila
kitu maana ajira zipo na hata wakija kwangu ninatoa ajira pia”,alisema mmoja wa
wajasiriamali hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake
Wakiongea kwa kusisitiza walisema wanawake
wanatakiwa kujishughulisha Zaidi kwa kuwa wanaweza na si kila kitu katika
kuendesha maisha wakamtegemea mwanaume tu.
Wanawake hao walielezea faida zinazopatikana ktokana
na kazi za ujasiriamali kuwa ni kukidhi mahitaji yao ya kila siku,kupata
umaarufu,kusaidizana majukumu na mwanaume na pia kujishughulisha kama mwanamke.
Aidha walibainisha changamoto wanazokutana nazo
kutokana na kazi hizo za ujasiriamali kuwa ni wivu baina ya wao kwa
wao,usumbufu na dharau kutoka kwa wateja na pia bwana afya kuwataka kuvalia
sare wakati wa kazi
“Changamoto tunazokutana nazo ni wivu kwa sisi wenyewe,bwana afya analazimisha
kuvaa sare,usumbufu kwa wateja na pia hawa wateja wetu hawatuheshimu
kabisa”,aliongea Bi. Maryam Abubakar
“Ushindani upo kila mahali ila kiukweli riziki inatoka kwa mungu na kila
mmoja ana fungu lake ila inatakiwa tuboreshe huduma zetu na kujituma pia”,
alieleza mama Soni
Kwa upande wa wateja wao wamelaumu hali ya usafi
katika mazingira wanayofanyia kazi na wakumbuke kuwa wanatoa huduma hiyo ya
chakula kwa binaadamu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa
wateja wa wajasiriamali hao Bi. Shadya Khamisi alisema huduma zao ni nzuri ila
hakuna budi kupewa semina ya usafi.
“Kiukweli huduma zao ni nzuri
kiasi lakini usafi haupo unakuta mtu anapika kichwa kikiwa wazi na vumbi la
magari na pikipiki linaingia kwenye vyakula ila ninaamini wakipewa semina ya
usafi itakuwa vizuri zaidi”, alishauri Bi. Shadya Khamisi
Mwisho kabisa waliwaahidi wateja wao kuwa wategemee
huduma bora zaidi kutoka kwao kwa vyakula bora na vyenye kujenga afya zao ila
tu waheshimiwe kama watu wanaofanya kazi zingine.
Habari
na Nassor Amour na Beatrice Mbowe
No comments:
Post a Comment