Thursday, 4 September 2014
BAADA YA EBOLA KUWA TISHIO UMOJA WA AFRIKA WAKUTANA KUJADILI...
Umoja wa Afrika (AU) umeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kukabiliana na kasi ya kuenea virusi vya homa ya Ebola barani humo. AU imetangaza kuwa katika kikao hicho kitachofanyika wiki ijayo kutajadiliwa njia za kuzuia kuenea virusi vya Ebola.
Hayo yanajiri huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema kuwa zaidi ya watu 1,900 wamefariki dunia huko magharibi mwa Afrika kutokana na ugonjwa huo. Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan amesema kuwa, wiki kii zimeripotiwa kesi 3,500 za ugonjwa wa Ebola huko Guinea, Sierra Leone na Liberia na zaidi ya vifo 1,900 tangu mfumuko wa ugonjwa huo uanze idadi ambayo bado inaongezeka.
Amesema kuwa, ana matumaini ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa katika kipindi cha miezi 6 hadi 9 ijayo.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa dola milioni 600 zinahitajika kwa ajili ya vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Ebola huko magharibi mwa Afrika. Wataalamu wanasema kuwa, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kimeongezeka na wiki iliyopita kuliripotiwa vifo vya watu karibu 400.
Habari Na Eliamini Mchome
Chanzo: Idhaa ya kiswahili ya Tehran
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment