Pichani: kulia ni Mratibu wa michezo katika chuo cha uhandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw Onesmo Elia Mbise akizungumza na mwandishi wa habari Geofrey Mashauri kutoka Ajtc Tv. |
Timu kutoka chuo cha uhandishi wa habari
na utangazaji Arusha{Ajtc stars &Ajtc queens}zimejipanga katika bonanza la
vyuo vya ufundi mkoani Arusha.
Akiongea na waandishi waaandishi wa habari
mapema leo ofisini kwake mratibu wa
michezo katika chuo cha uhandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw,Onesmo Elia
Mbise alisema kuwa wamepokea taarifa na wamejipanga vya kutosha.
Aidha
alisema kuwa kwa upande wa timu ya mpira wa miguu{AJTC STARS}imejipanga sana na
iko tayari hata leo kwani nidhamu ya mchezo imeshika nafasi hali kadhalika wana
mazoezi ya kutosha.
“kwa
upande wa maandalizi timu ya AJTC STARS ina maandalizi ya kutosha na imejipanga
vilivyo kukabiliana na timu yeyote hata leo
na kwa upande wa nidhamu sifa njema iwaendee kwa wachezaji kwani
wamekuwa na nidhamu bora”alisema mratibu huyo.
Hata
hivyo Bw.Mbise alieleza kwamba mazoezi ndio kitu ambacho walicho kikazania
haswa tangu walipo pata taarifa za mwaliko wa kushiriki bonanza hili,
“mchezaji
asiyefanya mazoezi hatacheza katika kikosi cha AJTC STARS na hata kama awe star
vipi,naamini mchezaji anayefanya mazoezi ndio atafanya vizuri zaidi na atakuwa
star”alisema Bw mbise.
Hata hivyo
kocha wa AJTC QUEENS Madam Eliesh Godson upande wa timu ya wanawake ambapo
halikadharika kaongelea suala la maandalizi kwa timu yake na maandalizi pia.
Pichani:Kocha wa Ajtc Queens Madam Eliesh Godson akizungumza na mhandishi wa habari Bw Hemedy Ismail kutoka Ajtc Tv. |
“Ajtc queens tumejiandaa kadri
tulivyo weza japo hata kwa siku mbili[2]wachezaji wanaweza kufanya mazoezi na
kucheza mechi,ila kwa sasa tuna wiki moja[1] hivi tangu tumeanza zoezi hivyo
tumejipanga sana”alisema Madam
Lakini changamoto ambazo zinaonekana
kuchukua nafasi kwa timu kutoka chuo cha uhandishi wa habari Ajtc ni pamoja na
wachezaji wengine kuwepo kenye likizo baada ya kufunga chuo,Ambapo wengi zaidi
katika upande wa Ajtc Queens.
“Wachezaji hawajatimia hii inaweza
kuwa changamoto kwetu japokuwa mpira wa pete unahitaji wachezaji saba[7]tu
kuunda kikosi cha kwanza na wachezaji wengine wamefunga chuo ila walio baki
wataitumikia timu”alisema Madam Eliesh Godson,
Pia
aliongelea suala la nidhamu kwa timu ya AJTC Queens kuwa ni kitu kilichopewa
thamani kubwa na nafasi ya kutosha,ambapo maamuzi yana utofauti kinidhamu .
“kwanza sifa ya kwanza ya mchezaji mzuri
wa mpira wa pete lazima awe na nidhamu na asiwe na kiburi,huu mpira wa pete ni
toufauti sana na mpira wa miguu kwani katika mpira wa pete mchezani anapo kosea
kinidhamua ataigharimu timu nzima inaweza isipate ushindi na mpira wa miguu
anapewa kadi nyekunda nab ado mchezo utaendelea”
Licha ya kubadirishwa kiwanja katika
mashindano haya ya Bonanza,Mr Onesmo hilo kwao si tatizo watacheza popote,awali
mashindano haya yalipangwa yafanyike katika kiwanja cha Shkh Amri Abeid Karume lakini sasa
yatafanyika katika kiwanja cha Oljoro Veta hapa jijini Arusha.
Pia katika Bonanza hilo kutakuwa na
mashindano mengine kama kukimbiza kuku,riadha kwa urefu mita 100-200,mita
400-800 kucheza muziki na mashindano ya kuimba.
Bonanza litahusisha Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Mkoa wa Arusha
ambapo mikoa hiyo itatoa timu za kucheza.
habari na(Geofrey mashauri&Hemedy Hamisi)
No comments:
Post a Comment