Afisa masoko wa chuo cha Uandishi uandi wa habari na
utangazaji Arusha Israel Mungule Kulia,Akizungumza na Mwandishi wa habari Prisca Mushi ofisini kwake mapema leo.picha na SALEHE ABDALLAH.
Habari na Prisca Mushi,,Picha na SALEHE ABDALLAH.
Afisa masoko
katika chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji arusha bwana Israel mungure amebainisha mbinu mbalimbali wanazo
tumia katika kukitangaza chuo hicho.
Akizungumuza na waandishi wa habari mapema jana katika
ofisa yake Bwana Mungure alisema kuwa wanatembelea shule mbalimbali za sekondari
na kuwatangazia wanafuzi wanao hitimu kidato cha nne na kuwa na sifa za ufaulu
ili kujiunga na chuo hicho.
Aidha alisema kuwa wanatumia vyombo mbalimbali vya
habari kukitangaza chuo hicho kupitia
radio safina,sauti ya injili moshi,radio 5, na nyingine nyingi kupitia
matangazo yanayorushwa kwa siku mara tatu.
Bwana;
mungure ameeleza pia kuwa wanatumia
mitandao ya kijamii kama face book,tuvuti,pamoja na barua pepe ili kuhakikisha
matangazo yao yanawafikia walengwa kwa wakati muafaka,
‘Pia
tunasambaza vipeperushi sehemu mbalimbali kwa ajili ya kukitangaza chuo chetu
kwa watu ’’alisema mungure.
Pamoja na
hayo mungure alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupata wanafunzi wengi kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro Tanga, Iinga Da es salaam
pamoja na mikoa jirani ya Arusha.
Alisema kuwa wanampango wa kuboresha majengo na miundombinu ili kupata wanafunzi wengi zaidi kutoka sehemu mbalimba za nchi na pamoja na nje
ya nchi.
Kutokana na
uchache wa madarasa katika chuo hicho Mungure amesema wanampango wa utafuta
eneo kubwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya
wanafunzi wote.
Sanjari na
hayo alibainisha changamoto wanazo
kumbananazo ni pamoja na gharama za matangazo kuwa juu kwa baadhi ya vyombo vya habari wanavyo
vitumia katika kukitangaza chuo hicho
”Gharama za matangazo
zipo juu na kwawakati mwingine tangazo
halipi gwi kwa wakati kama mkataba unavyo sema”alisema israei mungure.
Alimalizia kwa kuwashauri wazazi na walezi
kuwaleta watoto wao ili kupata elimu bora ya uandishi wa habari na
utangazaji kwani ni chuo hicho kina
shikilia nafasi ya pili kwa ubora hapa nchini kutokana na kuwa na walimu
bora studio za Radio na Tv za mafunzo kwa vitendo ili kuwa patia uzoefu wanafunzi wanao soma
katika chuo hicho.
No comments:
Post a Comment