Pages
Home
About us
Vision
Our tv
Tv program
Contact us
Classes and time table
Monday, 1 September 2014
MAWAZIRI WAPYA SIRYA WAAPISHWA...
Rais Bashar Assad wa Syria jana aliliapisha baraza lake la mawaziri huku akisisitiza kuwa, usalama na ujenzi mpya wa nchi hiyo ni vipaumbele vya serikali ya nchi hiyo. Sherehe za kuapishwa baraza jipya la mawaziri walioteuliwa mapema wiki hii, zilifanyika jana huko Damascus mji mkuu wa nchi hiyo. Wael al Halqi Waziri Mkuu wa Syria anaongoza baraza hilo jipya la mawaziri linalowajumuisha mawaziri wapya 11. Katika sherehe hizo za kula kiapo, Rais Assad wa Syria amesema kuwa mafanikio ya serikali mpya ya nchi hiyo yatategemea kuwa wazi serikali na kuaminiwa na wananchi. Bashar al Assad alichaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Rais wa Syria kwa muhula wa tatu katika uchaguzi uliofanyika mwezi Juni mwaka huu ambapo aliibuka na ushindi wa asilimia 88.7 ya kura. Syria imekumbwa na machafuko makubwa tangu mwaka 2011, huku nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo khususan Qatar, Saudi Arabia na Uturuki zikiwaunga mkono wanamgambo wanaozusha machafuko na kufanya mauaji huko Syria
Habari na Rosemary Mmbando
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment