Familia ya mwandishi wa habari
Steven Sotloff hatimaye imezungumza kwa mara ya kwanza tangu mtoto wao
auawe na wapiganaji wa dola ya Kiislam IS na picha za mauaji hayo
kuonyeshwa.
Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, Barak
Barfi kutoka taasisi ya America Foundation think tank akiwa nyumbani
kwao Pinecrest, Florida amemuelezea Sotloff kuwa ni mtu aliyefanya kazi
yake kwa niaba ya wanyonge wa Mashariki ya kati.
Wanafamilia hao wamesema mtoto wao hakuwa tu
shujaa bali ni wa namna yake ambaye daima alikuwa akitafuta kurejesha
nuru palipo na giza.
Hata hivyo wazazi hao wa Steven walitoa heshima
zao pia kwa kifo cha James Foley aliyechinjwa pia na wapiganaji hao wa
dola ya Kiislam ya IS. HABARI NA ROSEMARY MMBANDO. chanzo ni BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment