Tuesday, 9 September 2014

UJASIRIAMALI NDIYO MKOMBOZI WA MWANAMKE NCHINI

Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha kwa kufanyakazi za ujasiriamali na kuacha kuwategemea wanaume zao katika kuendesha maisha.

Wito huo umetolewa na wanawake wauzao chakula (mama ntilie) jijini Arusha walipokuwa wanaongea na mwandishi wa habari hizi mapema leo.

              ‘’Inatakiwa wanawake tujishughulishe tuache kumtegemea mwanaume kwa kila kitu maana ajira zipo na hata wakija kwangu ninatoa ajira pia”,alisema mmoja wa wajasiriamali hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake

Pichani; Baadhi ya vyombo wanavyotumia wajasiriamali hao (picha na Nassor Amour)
Wakiongea kwa kusisitiza walisema wanawake wanatakiwa kujishughulisha Zaidi kwa kuwa wanaweza na si kila kitu katika kuendesha maisha wakamtegemea mwanaume tu.

Wanawake hao walielezea faida zinazopatikana ktokana na kazi za ujasiriamali kuwa ni kukidhi mahitaji yao ya kila siku,kupata umaarufu,kusaidizana majukumu na mwanaume na pia kujishughulisha kama mwanamke.

Aidha walibainisha changamoto wanazokutana nazo kutokana na kazi hizo za ujasiriamali kuwa ni wivu baina ya wao kwa wao,usumbufu na dharau kutoka kwa wateja na pia bwana afya kuwataka kuvalia sare wakati wa kazi

                   “Changamoto tunazokutana nazo ni wivu kwa sisi wenyewe,bwana afya analazimisha kuvaa sare,usumbufu kwa wateja na pia hawa wateja wetu hawatuheshimu kabisa”,aliongea Bi. Maryam Abubakar

Pichani; MMoja wa waateja wa wajasiriamali hao (Picha na Nassor Amour)
Pia walieleza kuwa kuna ushindani wanaopeana lakini wameeleza kuwa riziki anatoa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila dawa pekee ya ushindani huo ni kujituma na kuboresha huduma zao.

                   “Ushindani upo kila mahali ila kiukweli riziki inatoka kwa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila inatakiwa tuboreshe huduma zetu na kujituma pia”, alieleza mama Soni

Kwa upande wa wateja wao wamelaumu hali ya usafi katika mazingira wanayofanyia kazi na wakumbuke kuwa wanatoa huduma hiyo ya chakula kwa binaadamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wateja wa wajasiriamali hao Bi. Shadya Khamisi alisema huduma zao ni nzuri ila hakuna budi kupewa semina ya usafi.

Pichani; Bi.Shadya Khamisi akielezea hali ya usafi wa mama ntilie jijini Arusha(picha na Nassor Amour)
                     “Kiukweli huduma zao ni nzuri kiasi lakini usafi haupo unakuta mtu anapika kichwa kikiwa wazi na vumbi la magari na pikipiki linaingia kwenye vyakula ila ninaamini wakipewa semina ya usafi itakuwa vizuri zaidi”, alishauri Bi. Shadya Khamisi

Mwisho kabisa waliwaahidi wateja wao kuwa wategemee huduma bora zaidi kutoka kwao kqa vyakula bora na vyenye kujenga afya zao ila tu waheshimiwe kama watu wanaofanya kazi zingine.


Habari na Nassor Amour na Beatrice Mbowe


No comments:

Post a Comment