Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa
Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.
HABARI NA MARIAM HIZZA
Mkutano huo ambao ufunguzi
wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto
zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi, na ambavyo nchi zaAfrika zitakavyoweza kunufaika
na rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na jangahilo.
Aidha Waziri mkuu Pinda
alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za bara la Afrika piautahusisha namna ambavyo
serikali za Afrika zinaweza kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko yaTabiachi. Pia alisema kuwa
mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadilikoya Tabianchi utakaofanyika
mjini Newyork Marekani unaotegemewa kufunguliwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa Bw. Ban KI
Moon.
“Wote tunafahamu kwamba
mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madharayake yanatofautiana kutokana
na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato” Aliongezakuwa kutokana na uchumi
tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi
kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadilikoya Tabianchi na kuwa na uchumi
mbovu.
Aliendelea kusema kuwa Afrika
na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa kisiasa katikakuungana kwa pamoja ili kuweza
kushirikiana katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimilina kukabiliana na athari hizo.
No comments:
Post a Comment