Wednesday, 13 August 2014

AJTC STARS YAJIPANGA KUENDELEZA UBINGWA.


(mwalimu wa michezo AJTC ndg Lucas Modaha)
HABARI NA 
    JESCA MHOKA, ARUSHA
Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC STARS) imejipanga kuendeleza ubingwa katika michuano mingine ijayo ndani na nje ya jiji la hilo.


Hayo yamesemwa na mwalimu wa michezo chuoni hapo Bwana Lucas Modaha mapema hii leo wakati alipotembelewa na AJTCTV katika ofisi yake iliyopo jijini Arusha.


Kwasasa AJTC stars inaongoza kwa kuchukua ubingwa kwa mara tatu mfululizo katika mashindano ya media bonanza yanayofanyika kila mwaka na kuchukua ubingwa wa kombe la Mandela linalojulikana kama Mandela Cup na ipo katika nafasi ya tatu katika mashindano ya kombe la Mbuzi huku nafasi ya kwanza ikishikwa na timu ya Filed force nay a pili ni Arusha sport.
(kutoka kushoto mwandishi wa ajtcblog Jesca Mhoka akizungumza na mwalimu wa michezo wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha ndg Lucas Modaha Picha na Johaness Johnson)
Licha ya kuwa na mafanikio hayo, Bwana Modaha amezielezea changamoto ambazo timu hiyo inakumbana nazo zikiwemo ukosefu wa fedha, vifaa na baadhi ya wanamichezo kutokuhudhuria mazoezini huku wakitaka kupangwa na kuendelea kuwepo kwenye timu.


“Tunaupungufu kidogo wa vifaa vya michezo, havitoshelezi, yaani havikidhi mahitaji ya timu kwa mfano kwa kawaida timu inatakiwa walau iwe na mipira kama kumi hivi kwa ajiri ya mazoezi lakini kwa sasa tuna mipira kama mitatu tu, tulikuwa na upungufu wa jezi tunashukuru tumepata za wasichana na wavulana na mchezaji anapokuwa kambini anahitaji apate walau chai lakini tunashindwa kwasababu hatuna fedha” alisema Lucas modaha


Mwalimu Modaha ameongoza kwa kusema kuwa chuo kinatoa fursa kwa wachezaji ambay wanaichezea timu hiyo ikiwemo kusomeshwa kozi mbalimbali bure kwa anayependa kusoma na kumhudumia mchezaji  atakaye patwa na majeraha wakati akiwa uwanjani.
kikosi cha AJTC STARS

“Kwa mchezaji yeyote atakaye umia akiwa uwanjani achana na akienda kwenye michezo yake ya ndondo ya mitaani, sisi kama viongozi wa chuo na mimi nkiwa mwalimu wa michezo nitasimamia kuwa huyo mtu anapatiwa huduma zote zinazotakiwa na hatutagusa fedha zake za matibabu na atatibiwa bure kabisa.”

Bwana Lucas amemaliza kwa kutoa ushauri kwa wachezaji waache kulalamika, wafanye mazoezi kwni mazoezi ni hujenga afya, husaidia kuepuka kushambuliwa na magonjwa na kuwa na akili yenye uwezo wa kufikiri kwa haraka zaidi.


 

No comments:

Post a Comment