wasanii wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili kulia ni Rais wa bendi Nyoshi
Rapa wa bendi ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo
Wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini wote hawa watakuwepo katika uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa.
HABARI NA GEOFREY MASHAURI
Fm
Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani kuanzia mwaka
2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua rasmi album mpya kabisa
inayojulikana kwa jina la Chuki ya nini ndani ya jiji la Arusha na
vitongoji vyake .
Album
ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo ni:-Chuki ya nini,
Fataki ,Otilia ,Ndoa ya kisasa,Neema,Dai chako
ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni album yenye
kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote zitazinduliwa rasmi
septembar tano mwaka huu ndani ya viwanja vya ukumbi wa Triple A jijini
Arusha
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB Intamenti Seif
Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa
kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu wa albamu mpya ambapo alibainisha kua
tukio hilo litakuwa la kihistoria.
Alisema
kuwa hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii kuzindua albamu nje ya mkoa
wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua kuwapa heshima kubwa wapenzi wa
bendi hiyo wa mkoa wa Arusha pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa
ujumla hii ikiwa ni heshima ya kipekee.
"uzinduzi
huu wa albamu sio tu tunazindua nyimbo mpya bali tunazindua pia
vyombo vipya na staili mpya za kuicheza gwasuma kama vile mnavyojua
bendi ya fm ni wazee wa pamba wazee wa kushambulia jukwaa"alisema
Manyota
Aidha
alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa kipaumbele na pia
kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma wameamua kufanya shoo hii nje
ambapo ,kutafugwa jukwaa la kisasa kabisa.
Alitaja
baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo inazinduliwa kuwa ni
pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya kisasa fataki pamoja na nyinginezo.
Aidha
kwa upande mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha tu bali
wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii na kuzitambua staili
mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo kwenye albamu hii.
Alisema
kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya iliyozinduliwa huku
akisema kuwa kwa upande wa Arusha kiingili akuwa 20000 na unapatiwa
CD moja buru mlangoni.
kwa
upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu yake yote
imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha na kuwapa
staili mpya ikiwemo ile ya vundesa ambapo alisema kuwa wameiboresha na
imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu
pamoja na maneno matamu.
Alisema
kuwa lengola kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini Arusha ni pamoja
na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao
wanajua staili zao zote za nyimbo hizo na sio ivyo tu pia alisema kuwa
kwa kipindi hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea
wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32 na wote watafika
jijini Arusha
No comments:
Post a Comment