Friday, 29 August 2014

UNAJUA KAMA KILA BINGWA ANA BINGWA WAKE? SOMA HII


MABINGWA MARA MBILI MFULULIZO WA KOMBE LA      TASWA WAPIGWA MVUA YA MABAO 

habari na NASSOR S AMOUR 

Mabingwa wa kombe la taswa kanda ya kaskazini ambao ni chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) wamemiminiwa mvua ya magoli matatu kwa mbili na timu ya SOMBETINI PARISH FC mapema wiki hii.

 Mtanange huo ambao umepigwa mida ya saa kumi za jioni katika viwanja vya FFU Arusha umezikutanisha timu hizo mbili katika robo fainali ya kombe la NANI ZAIDI lililojumuisha timu kama AJtC stars,Sombetini Parish fc,FFU na zingine kibao.
Ikiwa na mchezo wa sita kwa kila timu Sombetini Parish imejiwekea rekodi ya kutofungwa mechi hata moja katika ligi hii wakiwa wameibuka na ushindi wa michezo mitatu na suluhu katika michezo mitatu waliyoweza kucheza.

Na timu ya Ajtc stars imeweza kushinda michezo mitatu,sare mchezo mmoja  na kuchabangwa katika michezo miwili waliyoweza kucheza katika ligi hii,matokeo yamchezo huo umeitoa timu ya Ajtc stars katika mashindano na kuiruhusu Sombetini parish kuingia katika nusu fainali ya ligi hii.

Mabao katika mchezo huo,Ajtc stars ilianza kwa kutupia goli kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na mshambuliaji wa timu hiyo Fred ’16 dakika ya tatu ya mchezo huo ambae pia alirudi golini na kutupia bao la pili katika dakika ya tisini ya mchezo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFeEmnZaNYoTjfvRrbDTWlifIljmBXQe17EQlEVh1lX6OadqidtLIuoqjC2NERYR6tp5PMEMkezsp025ArtOuNiZbm8hBcwtQnqe81GIAIBFp3rxHDdXV8wFlOgfciar6VUlw3on_Vc8lD/s1600/4.jpg
Pichani ni baadhi ya wachezaji wa Ajtc stars
 Kwa upande wa washindi wa mchezo huo Sombetini Parish  mabao yaliwekwa kimyani na Emmanuel ’11 katika dakika arobaini ya mchezo,bao la pili kupitia nahodha wa timu hiyo Sam Petro dakika arobaini na tano ya mchezo na kapu la  mabao lilihitimishwa na Frank Ally kupitia mkwaju wa penati dakika ya sabini ya mchezo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOEq3BjL_g6uGbn_E1z0QzofmJXiFl7I3GeWnE0qsYc2wt8hYcsTmi9IGH8VeVul5qUiOtz89kohLJ5vTw74v5WGugFkIs847BYz-Ia65B85KjPDZNUYh2RG1vsbr2bW_ZErDOoLmCXkMB/s1600/1.jpg
(Pichani) Kocha wa AJTC stars bwana Idrissa Bakari akiongea na wanahabari uwanjani Field force




 Mchezo huo ambao timu hizo zilionyesha kukamiana na kila mmoja kutaka kulichungulia lango la mwenzie ila Sombetini iliibuka kidedea kwa mabao 3-2 dhidi ya Ajtc stars.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kocha wa timu ya Ajtc stars amesema huo ni moja ya mchezo sababu kuna kushinda,kushindwa na suluhu na kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwake,Pia akaongezea kusema japo watu wanamlaumu kuchezesha mamluki katika kikosi chake akasema hayo ni maneno ya mashabiki tu. 

           “unajua kushindwa,kushinda na suluhu ni moja ya mchezo na kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwangu na siwezi kuwa ‘’BLAME’’ wachezaji wangu wameshindwa kutengeneza ‘’chemistry’’ ya mchezo na nahitajika kujipanga kwa michuano mingine kuhusu mamluki hao ni mashabiki tu wanaongea hivyo”,alisema kocha Idrissa Bakari

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmNkbYjFs1CWKH3CvqHi-43UweocC2uC-A6KAePpYK5AEd9NXnP6NkftE6CbLJu9olqxXx69C9pe9YFQr4MAHODVOFq9-Xo7XkiF-azvNZWtIwKMcsaPN41oSjqFin7pSNgH7pkTSYn_JP/s1600/2.jpg
Pichani Mwenye suti nyeusi Kocha wa Sombetini bwana Kamanda akitoa ufafanuzi juu ya mchezo wa leo kwa waandishi wa habari

Nae kocha wa Sombetini Parish amesema ushindi huu ulikuwa ni wa lazima kwao kutokana na maandalizi ya michuano hiyo waliyoyafanya kuanzia mwanzo na wamejipanga vizuri katika kuingia katika nusu fainali ya michuano hiyo na amelaumu kwa wachezaji wake kupewa kadi zisizo za lazima.

         ‘’Yaa ushindi wa leo ulikua ni wa lazima kwetukutokana na maandalizi katika mashindano haya tuliyoyafanya tokea mwanzo na tumejipanga vizuri kwa kufanya mazoezi na leo tumepewa kadi zisizo za lazima ila si kwamba timu haina nidhamu’’,alisema kocha Kamanda.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKs1lHGX5631AAuwYue-ln6299-V_QU1ZOSohQpCs5BaPDue1jj8A1IU6L2qsl_Xb_-AUfjnKGzK8DgmiN4UWlZ-BARm4vER_GLxxiB1HLf8ZkjcJgqQn2qtpPC-xnPym8U_6qLSyzg8BF/s1600/5.jpg
Pichani mashabiki wa Sombetini Parish wakisherehekea ushindi dhidi ya Ajtc stars

 Ushindi wa huu umewapa nafasi Sombetini Parish kuwa na mchezo siku ya ijumaa na wanasema wamejipanga vyema katika kuingia kwenye mchezo huo na kuahidi ushindi kwa timu hiyo.

Pia mwandishi wetu aliweza kuongea na mashabiki wa timu zote mbili na kusema timu zo zimecheza vilivyo na matokeo yaliyotokea ni moja ya mchezo na wameahidi kuendelea kuzishabikia timu zao.


No comments:

Post a Comment