Wednesday, 13 August 2014

BURUDANI KATIKA MUZIKI KITAIFA :: WASANII WAAASWA KUWA NA UMOJA NA USHIRIKIANO ILI KUFIKA NGAZI ZA KIMATAIFA .

Wasanii wa muziki nchini Tanzania waswa kuwa na ushirikiano ili kuweza kuupeleka na kuutangaza muziki wa hapa nyumbani duniani kote .
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Masha G.M.G
Hayo yamesemwa na msanii chipukizi toka nchini Tanzania MASHA G.M.G aliyazungumza hayo wakati akifanya mahojiano na AJTC TV.BLOGSPOT.COM .
Hitmaker wa ngoma ya MONEY pia alizungumzia kuhusu ushirikiano hafifu kwa wasanii hapa nchini kwani wasanii wanaridhika na kujisikia.
Kutoka kushoto ni mwandishi wa habari hii na msanii Masha.

“Unaenda studio kufanya muziki mzuri na unaona kabisa kwenye mdundo huo [BEAT] msanii Fulani anaweza kuingiza voko ama sauti lakini unapomtafuta msanii huyo anakwambia hawezi kufanya mziki shirikishi na msanii chipukizi”alisema,Masha.

Pia masha alisema muziki utafanyika kama nchi za nje utaweza kubadilisha maisha ya wasanii pamoja ma mitizamo ya wasanii kwani wasanii wa nchi za nje wanaushiriano na kuthamini wanachokifanya .

“Wenzetu bhana nje wanajua wanachikifanaya na kukithamini ,so tukibadilika tutaweza kufanya muziki kama wenzetu sababu wao wanalijua soko “alisema,Masha.

Masha ambaye tayari amekwisha kufanya kazi na wasanii kama vile COUNTRY BOY,NIKKI MBISHI, JAY RIDER toka tongwe records pamoja na wasanii wengine kibao.

Hata hivyo MASHA alimalizia kwa kusema kuwa kwakuwa kuna umioja wa wasanii nchini tutaweza kukaa na kupanga mipango mizuri kwa ajili ya kufanya na kuendeleza muziki hapa nyumbani. >> HABARI NA  NA PICHA NA JOHANESS KINANILA  





No comments:

Post a Comment