Mwalim David Pallangyo akitoa maelezo kuhusu wanafunzi kusoma kwa bidii katika chuo ualimu Arusha
huku mwandishi wetu Linah Mvungi akiandika maelezo yake (Picha na Irine Lymo)
Na.Linah Mvungi
Mkuu wa kitengo cha elimu ya uwalimu wa awali David
Pallangyo amewashauri wanafunzi watilie
mkazo kwa kile wanachofundishwa na kuwa makini pindi mwalimu
afundishapo.
Hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari
wa ajtc redio waliofika chuoni hapo
mapema hivi leo.
Kitengo hicho ambacho mwanzoni kilioanza kutoa elimu ya sekondari kwa mwaka
2011 ,2012 lakini mpaka kufikia mwaka 2013
ndipo walipoanzisha elimu ya
uwalimu wa chekechea kwa ngazi ya cheti cha awali
lakini kwa mwaka huu wamefanikiwa kuwa na darasa la ngazi ya stashahada.
Pallangyo alisema
kuwa Jpo wamefikia hapo ila wana changamoto
zinazowakumba ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa
madarasa yao binafsi hali
inayowafanya muda mwingine kukosa madarasa ya kufundishia.
Pia aliwashauri wanafunzi kujua kile
wanachokifanya ili kuweza
kushindana na soko la ajira na pia walimu
waongeze juhudi katika
kufundisha na ustadi mpya
ili kuwafanya wanafunzi kuwa na
uelewa mkubwa.
No comments:
Post a Comment