Kikosi cha AJTC stars (Picha na charles chami) |
Kocha wa timu ya A.J.T.C
stars Idrisa Bakari amethibitisha rasmi
kwamba timu yake itaendelea kuwania kombe la nani zadi cup linaloendelea
kushika kasi katika kiwanja cha fid foce kwa morombo hapa jijini arusha
Kulia ni kocha wa AJTC stars Idrisa Bakari akifanyana mojiano na mwandishi wetu Charles chami jana (Picha na Rajabu kibakaya ) |
Awali mabingwa hao wa taswa mkoa wa arusha
walitangaza kujitoa katika michuano hiyo baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya
mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Fid Force FC wakidai kuwa aliwapa wapinzani wao
goli la kuotea katika mchezo waliotoka pua chini wakilala kwa kipigo cha goli
moja kwa bila
Maamuzi hayo yamekuja baada ya baadhi ya waratibu wa
michuano hiyo kuonana na uongozi wa michezo pamoja na kocha wa AJTC kuwaomba
warudi katika michuano hiyo inayoshirikisha timu 16 na kuwapa masharti matatu
moja mchezo wao dhidi ya Fid force urudiwe pili mchezo huo upigwe katika dimba
la shekh amri abeid na tatu kama
autarudiwa katika dimba hilo watafute mwamuzi mwingine pamoja na washika
vibendera
Ratiba ya michuano hiyo inaonyesha kuwa mchezo ujao
wanachza na katika dimbaa hilo la fid force kocha wa AJTC Akizungumzia mchezo
huo amesema kuwa vijana wake wako vizuri kisakologia kwaajili ya mchezo wowote
ambao watakutana nao mbele yao.
Baada ya mchezo huo watakuwa wamebakiwa na mchezo
mmoja katika kundi A kabla ya kubakia timu nne zitakazotinga hatua ya robo
fainali
Bingwa wa kombe hilo la nani zaidi cup ataibuka na
mbuzi mnyama mwenye dhamani ya laki mbili taslimu za kitanzania Habari na CHARLES B. CHAMI
T.B.T
ReplyDelete