Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment