Arusha
Na Olimpia Mallya
Wito umetolewa kwa wafunzi wa chuo
cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) kujikita zaidi katika masomo
yao ili kufikia malengo yao yaliyowaleta chuoni hapo.
Rai hiyo imetolewa na mwalimu mlezi
wa wafunzi chuoni hapo Neema Ezekieli Mwaipela wakati akizungumza na mwandishi
wa habari ofisi kwake kuhusu maendeleo ya wanafunzi chuoni hapo.
Mwalimu mlezi wa
wanafunzi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Neema Ezekieli Mwaipela akizungumza
na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.
(picha na Grace Mboya)
Hata hivyo alisema kuwa utoro umepungua kwa kiasi kikubwa
kulinganisha na kipindi cha nyuma ambapo wanafunzi waliowengi walikuwa
wakishuka kiwango cha ufaulu kutokana na kukosa vipindi darasani na kunyimwa kufanya mitiani ya
mwisho wa muhula kwa kutokuwa na sifa zinazo hitajika .
Akizungumza mienendo ya wanafunzi
alisema kuwa baadhi yao wamekuwa
wakijichukulia maamuzi ya kupeleka kesi mbele
ya sheria bila kuhusisha uongozi wa chuo na kuwaomba wasifanye hivyo kwani
kufanya hivyo ni kuudharau uongozi wa chuo.
“Unakuta wanafunzi wenyewe
wamekoseana au wamechukuliana vifaa kama vile laptop ,kamera wakashindwa kulipana wanahamua kufikisha kesi
mahakamani bila uongozi wa chuo kufahamu
huu ni utovu wa nidhamu na hugharimu uongozi wa chuo kufuata kesi
mahakamani kuirudisha kwenye uongozi wa chuo”Alisema Neema Mwaipela mwalimu
mlezi wa wanafunzi chuoni hapo.
Alisema changamoto kubwa iliyokuwa
ikiwakabili wanafunzi kuwa wajawazito pindi wakiwa kwenye masomo na kusema kuwa
imepungua kwa kiasi kikubwa baada ya semina kutolewa.
“Baada ya kutoa semina kwa wanafunzi
wakike kuhusu kujielewa au namna kuepukana na mimba wakiwa masomoni imeonesha
manufaa kwetu kwani idadi ya wajawazito imepungua sana”Alisema Mwaipela.
Kwa upande wa wanafunzi wa kike
chuoni hapo wametoa shukrani za dhati kwa uongozi wa chuo kwakuwapatia semina
mbalimbali kwani zimewasaidia kufahamu mambo mengi waliyo kuwa hawafahamu.
ajtctv.blogspot.com
ajtctv.blogspot.com
No comments:
Post a Comment