Tuesday, 12 August 2014

WANAFUNZI WA A.J.T.C WATAKIWA KULIPA ADA KWA WAKATI

Makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bwana Elifuraha samboto amezungumza mwandishi wetu Hadija Hassan (Picha na Nassoro Amour)

Makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bwana Elifuraha samboto amezungumzia swala la ulipaji ada kwa wakati unao takiwa

Akizungumza na mwandishi wa habari bwana samboto ofisini kwake amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa hawalipiada kwa wakati unaotakiwa
Ameendelea kwa kusema kuwa hawana njia yeyote ya kuwasaidia zaidi ya kuwarudisha nyumbani mpaka watakapo pata ada na hivyo kupelekea wanafunzi kukosa masomo
Pia amezungumzia changamoto wanazozipata wakati wa kuwarudishwa ada kwa wanafunzi kama vile wengi hawafuatiutaratibu wa ulipaji ada na wengine hawalipi kabisa

Amemalizia kwa kusema kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kulipa ada kwa muda unaotakiwa ili kuepuka usumbufu wa kurudishwa nyumbani na kukosa masomo. HABARI NA HADIJA HASSAN

No comments:

Post a Comment