Kwa mara ya kwanza sasa vipindi vya ajtc tv vyaanza kuruka hewani hii ni kutokana na maendeleo mazuru ya chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji arusha(AJTC).AJTC TV ni kitengo cha Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji ambacho hutumika katika kuwa andaa wanachuo katika mazoezi ya vitendo kwa kuandaa Vipindi mbalimbali vya Television ambavyo wamekuwa wakianda vipindi vya Live na Recorded.
|
Nurudin Paul akitangaza taarifa ya habari ndani ya chumba cha utangazaji cha ajtc tv |
"Tumeamua kuanzisha AJTC TV online kwa sababu uwezo wa wanachuo wetu umekuwa mkubwa sana kiasi cha kuweze kuandaa vipindi vyenye ubora na vilivyo tengenezwa kitaalamu kiasi chakuweza kuwafanya Watanzania milioni 45 kuvitazama na kuelimika pia kuburudika,pia tunataka tuwandae wanachuo walio bora na watakao toka wakiwa na uzoefu mzuri,hadi hivi sasa wameweza kuanda vipindi vingi na wanaendelea kuanda kila siku,Na napenda kuwaomba wazazi na walezi pia na mashirika kutazama ajtc tv katika blog yetu na pia you tube ili kuona vipindi vinavyo andaliwa na watoto wao."Alisema Mwalimu wa Kitengo cha AJTC TV bwana Isaac Chiwanga.
|
Roda Kimathi akitangaza kipindi cha burudani cha Uwanja wa raha cha ajtc tv |
Pia ajtc tv unaweza itazama kupitia YOU TUBE kwa kuandika AJTC TV hapo itakuletea mtililiko mzima wa vipindi vyetu vyote.
No comments:
Post a Comment