Habari na Mariam Hizza,
Wakufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha
{A.J.T.C} wametoa semina ya siku tatu kwa wanafunzi wake iliyomalizika mapema
leo chuoni hapo.
Wakitoa semina hiyo baadhi ya wakufunzi
wa chuo hicho waliwasisitiza wanafunzi pamoja na watu wengine kujihusisha na
ujasiliamali ili kuondokana na lindi la umaskini.
Akizindua semina hiyo mkuu wa chuo
hicho bwana Joseph mayagilla alitoa maada iliyowafundisha wanafunzi ni jinsi gani wanaweza kuhifadhi
pesa zao ili kufikia malengo na kuwa wajasiliamali wakubwa.
,, Unatakiwa ujue
kuhifadhi pesa zako na uwe na uelewa ipi ni pesa mazao na ipi ni pesa mavuno
hii itakusaidia kujua
jinsi ya kugawanya fedha zako.Alisema bwana Mayagilla.
Mratibu wa semina hiyo bwana Andrea
Ngobole aliwaasa wajasiliamali kujiwekea misingi katika biashara zao ili
kuepuka hasara zinazoepukika.
Bwana
Ngobole alisema kuwa ukitaka kuwa mjasiliamali inatakiwa uzingatie maadili ya
ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kuwajali na kuwaheshimu wateja wako na watu
wote kitu kitakachokuongezea wateja.
,, Ukiwa
mjasiliamali unatakiwa kuwa mvumilivu pia unatakiwa kuzingatia maadili ya kazi
yako na maadili kwa biashara yako
mwenyewe.Alisema bwana Ngobole,,
Licha ya kutoa semina pia ilitolewa burudani iliyofanywa na
walimu pamoja na wanafunzi lengo likiwa ni kuburudisha pamoja na kuleta usikivu
kwa wasikilizaji.
Makamu mkuu wa
chuo hicho bwana Elifuraha Samboto alihitimisha kwa kuwashukuru wote
waliohudhuria semina hiyo pamoja na kuwasihi wawe na tabia ya kujisomea vitabu
na kuhudhuria semina ilikuongeza ujuzi na kujua changamoto wanazopata
wajasiliamali wakubwa na jinsi ya kukabiliana nazo.