Friday, 3 October 2014

UJASIRIAMALI KURAHISISHA MAISHA.....ARUSHA

                  Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Adson Kagiye Mayagila                   akiwasilisha mada katika semina ya Ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo mapema hii                      leo.Picha na Mariam Hizza.

   Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mafunzo   ya semina ya Ujasiriamali katika ukumbi wa chuo hicho hii leo.Picha na Mariam Hizza.

Wakufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha ambao pia walikuwa ndio wawasilishaji wa mada za semina ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja.Wa tatu kutoka kushoto waliokaa ni Makam Mkuu wa Chuo,Elifuraha Samboto.Picha na Mariam Hizza.

Habari na Mariam Hizza,
 Wakufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {A.J.T.C} wametoa semina ya siku tatu kwa wanafunzi wake iliyomalizika mapema leo chuoni hapo.
  
Wakitoa semina hiyo baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho waliwasisitiza wanafunzi pamoja na watu wengine kujihusisha na ujasiliamali ili kuondokana na lindi la umaskini.

 Akizindua semina hiyo mkuu wa chuo hicho bwana Joseph mayagilla alitoa maada iliyowafundisha  wanafunzi ni jinsi gani wanaweza kuhifadhi pesa zao ili kufikia malengo na kuwa wajasiliamali wakubwa.
   ,, Unatakiwa ujue kuhifadhi pesa zako na uwe na uelewa ipi ni pesa mazao na ipi ni pesa mavuno 
     hii  itakusaidia kujua jinsi ya kugawanya fedha zako.Alisema bwana Mayagilla.

  Mratibu wa semina hiyo bwana Andrea Ngobole aliwaasa wajasiliamali kujiwekea misingi katika biashara zao ili kuepuka hasara zinazoepukika.

Bwana Ngobole alisema kuwa ukitaka kuwa mjasiliamali inatakiwa uzingatie maadili ya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kuwajali na kuwaheshimu wateja wako na watu wote kitu kitakachokuongezea wateja.
   ,, Ukiwa mjasiliamali unatakiwa kuwa mvumilivu pia unatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yako          na maadili kwa biashara yako mwenyewe.Alisema bwana Ngobole,,

 Licha ya kutoa semina pia ilitolewa burudani iliyofanywa na walimu pamoja na wanafunzi lengo likiwa ni kuburudisha pamoja na kuleta usikivu kwa wasikilizaji.

Makamu mkuu wa chuo hicho bwana Elifuraha Samboto alihitimisha kwa kuwashukuru wote waliohudhuria semina hiyo pamoja na kuwasihi wawe na tabia ya kujisomea vitabu na kuhudhuria semina ilikuongeza ujuzi na kujua changamoto wanazopata wajasiliamali wakubwa na jinsi ya kukabiliana nazo.
  

Wednesday, 1 October 2014

Semina ya ujasiliamali ndani ya chuo cha uandishi wa habari Arusha ya toa fursa.

Na.ELIZABETH SAID ADYSWELE

Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Akifungua semina ya ujasiriamali mapema leo. NA ELIZABETH SAID
















Mkurugenzi wa chuo chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha bwana Joseph Mayagila amefungua semina ya siku tatu ya ujasiriamali leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
Bwana Joseph Mayagila amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya ujasiriamali.
Alisema kuwa ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima ajue kupanda mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya kupanda mbegu.
“Unaweza kuhangaika sana kwa lengo  la kupata fedha mbegu, kwa kuwa mbegu hizo zitazalisha fedha nyingi zaidi kupitia mbegu hiyo”
Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni hapo ikiwemo kozi ya uandishi wa  habari, ualimu,sekretari pamoja na kozi ya kompyuta.
Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya mikakati ya kibiashara,  na mada ya huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo bw, Adrea Ngobole.  
Bwana Maygila alisema kuna kuuuza na kununua lakini sio kila mtu anaweza kuuza na kuwataka wote kujenga fikra zao katika kuuza ila waweze kujenga maisha yao
Alisema kama mtu anataka kufanikiwa maishani na kutaka kununua vitu vya thamani ni lazima mtu ajipange vizuri katika  kuuza
“Duniani kuna kuuza na kununua huwezi kukwepa kununua lakini  sio kila mtu anaweza kuuza, unaweza kuuza mawazo, jambo na bidhaa” Alisema Mayagila
Mayagila aliwashauri wanafunzi wake kujiunga   kwenye taasisi za kifedha kwani mkopo ni fedha mbegu na zitawasaidia  kufanikisha biashara zao na kuzaa zaidi
Amehitimisha ufunguzi wa  semina hiyo kwa kusema kwamba ili mtu yeyote afanikiwe ni lazima kusoma vitabu mbalimbali 
“Nyumba isiyyo na vitabu ni mfu, akili isiyopenda kusoma ni mfu pia ,ili uweze kufanikiwa nilazima ulipe gharama za kufanikiwa”
Na baada ya uzinduzi huo semina ilianza rasmi  ambapo Bw. Onesmo Mbise alifundisha maada ya Bussiness Planing na kuzungumuzia zaidi mikakati mahususi kuhusu biashara

                           Bw. Onesmo Elia Mbise, Akitoa mada

        

 Mkufunzi wa pili Bw. Christian Ndege yeye alifundisha somo la Customer Care na kueleza mbinu mbalimbali za kuvutia wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri , kumheshimu na kumtambua kuwa ni bosi na kumwomba radhi pale tu unapomkosea
Nae kwa upande wake Bw. Andrea Ngobole aliwasilisha somo la tatu kwa siku ya leo kuhusu misingi/miongozo ya mjasiriamali Bw. Ngobore amesema mjasiriamali yeyote ni vyema kuwa na marafiki  wajasiriamali ili kufanikiwa kupata taarifa mbalimbali kuhusu Biashara

                                  Bw. Andrea Ngobole Akiwasilisha maada                                                                    

Wakati huo huo pia ametaja mambo ambayo mjasiriamali anapaswa kuyaepuka  ikiwa ni pamoja na kulaumu, starehe, kuamini uchawi, umbea na mengine mengi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kufika mbali na kufanikiwa kibiashara


Baadhi ya wanafunzi wa kiwa katika semina chuoni hapo

Aidha wanafunzi walio wengi chuoni hapo wameipoke kwa furaha semina hiyo ambayo
            itaendelea tena mapema kesho asubuhi saa 3 kamili


Wednesday, 10 September 2014

UCHAFU KATIKA SOKO LA MBAUDA WAWAKERA WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO HILO.

 Hali isivyo ya kuridhisha katika soko la mbauda lililoko mkoani Arusha katika kata ya sombetini kutokana na kutapakaa kwa uchafu.   picha na Rosemery Mmbando.

          
  Wafanya biashara katika soko la Mbauda mkoani Arusha wameulalamikia uongozi wa kata ya sombetini lilipo soko hilo juu ya uchafu unaoletwa na wakazi wa jirani na soko hilo.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Mikaeli Materu amesema kuwa uchafu wa soko hilo unachangiwa na majirani wa soko hilo kuleta takataka kutoka majumbani mwao.

                 Bwana Mikaeli Materu akitoa maelezo wakati akizungumza na muandishi wa habari sokoni                    hapo . Picha na Rosemery Mmbando.

Bwana Materu ambaye ni mfanya biashara wa sokoni hapo tangu miaka ya 1990 amesema uchafu kama nywele na ngozi za wanyama ni uchafu usiozalishwa sokoni hapo lakini utaukuta katika mazingira ya soko hilo.
Akibainisha changamoto nyingingine bwana Materu amesema ukosefu wa mtaro wa maji taka sokoni hapo ni kero ambayo inawasumbua na hujitokeza zaidi katika kipindi cha mvua.
Pamoja na kuwa na kero hizo Bwana Materu amesema licha ya wenyeji na uzoefu alionao sokoni hapo hatambui kama kuna uongozi wa soko au lah.

                        Mpangilio mbovu wa wafanya biashara na mazingira machafu katika soko la mbauda                                       mkoani Arusha.  Picha na Rosemery Mmbando

Juhudi za kumpata diwani wa kata ya sombetini Bwana Ally Bananga hazikufanikiwa kutokana na kutokuwepo katika ofisi ya kata hiyo.Bwana Materu alimaliza kwa kuuomba uongozi wa kata hiyo na halmashauri kuboresha mazingira ya soko ili kupunguza msongamano wa wafanya biashara katikati ya jiji la Arusha.

                 Biashara zikiendelea sokoni hapo bila ya kujali hali ya usafi wa mazingira yenyewe
                 Picha na Rosemery Mmbando.

Soko la Mbauda katika kata ya Sombetini mkoani Arusha si soko rasmi lakini hata hivyo limekua msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.

                              Habari na; Eliamini Mchome na Rosemery Mmbando.

ARUSHA;SALUNI NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE..........

Mmiliki wa saluni mama Sundy akimuhudumia mteja wake.picha na MARIAM HIZZA. 


 
Kutuka kushoto ni mwandishi wa gazeti la ajtc akimuhoji mmiliki wa saluni iliyoko kwa morombo Arusha mama Sundy mapema leo.picha na MARIAM HIZZA.


Mteja akiwa saluni kwa mama Sundy akihudumiwa.picha na MARIAM HIZZA.

Habari na MARIAM HIZZA,
Wafanyakazi wa saloon wamelalamikia wateja wao ambao wana tabia ya kutaka kupunguziwa bei ambayo inakuwa ndogo ukilinganisha na maisha yalivyopanda kwa sasa.

  Akizungumza jana na mwandishi wetu mmoja wa wafanyakazi wa saloon iliyoko arusha maeneo ya kwa morombo aliyejitambulisha kwa jina la mama Sundy alisema kuwa wateja wake wajaribu kuangalia na hali ya maisha yalivyo.

 Mama huyo alisema kuwa licha ya wateja kutaka kupunguziwa bei pia wakikataa huwa wanahama na kuenda saloon nyingine kitendo ambacho kinawapunguzia wateja. 
                 “Utakuta mteja anataka apunguziwe bei na ukiangalia bei wanayotaka ni ndogo sana ukilinganisha na maisha                       ya sasa yamepanda yako juu sana”alisema mama Sundy.
Hata hivyo mama sundi alisema inabidi wateja ifike kipindi wawe waelewa kwani hela hiyohiyo  hutumika kulipia vyumba na hata kutumia kwa ajili ya mahitaji ya familia.
  Wateja walisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wateja wamekuwa na tabia hiyo ambayo hurudisha nyuma maendeleo.
Mmoja wa wateja hao aliyejitambulisha kwa jina la Halima alisema kuwa wapo baadhi ya wateja wenye tabia hiyo na kusema kuwa wawe wanawaonea huruma kwani hali ya maisha kwa sasa ni ngumu.
                 " Wateja tunatakiwa tuiheshimu kazi ya saloon na kuiona ni kazi kama kazi nyingine   tujaribu kuwaonea                                huruma kwani nao wana familia zinazowategemea”alisema bi Halima.
 Mama sundy alimalizia kwa kusema ifike kipindi watu wakubali kazi za watu na kuziheshimu kwani kufanya hivyo kutasaidia maisha kuwa mepesi hali ambayo itasaidia kupunguza umaskini hapa nchini.
   


BIASHARA YA NYAMA YA MBUZI YASHAMIRI JIJINI ARUSHA



kutoka kushoto ni muuzaji wa nyama yambuzi Bw.Rafael Isaya aakizungumza na mteja maeneo ya kwa Morombo Arusha

Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama katika soko la kwa morombo lililopo mkoani arusha wameeleza jinsi wanavyonufaika na kazi hiyo ya uchomaji wa nyama ya mbuzi.


Akizungumza na waandishi wahabari mmoja wa wafanyabiashara hao Bw.Rafaeli Issaya amesema kuwa,biashara ya uchomaji wa nyama ya mbuzi imemnufaisha kwa kiwango kikubwa cha maisha yake na familia yake.

Amesema kuwa nyama hiyo ya mbuzi iliyochomwa kiasi cha kilo moja huuzwa kwa bei ya shilingi elfu sita wakati mguu uliochomwa wennye kilo mbili huuzwa kwa shilingi elfu kumi.

Pia Bw.Rafaeli amesema kuwa kwa siku za kawaida huchinja mbuzi wawili hadi watatu lakini kwa siku za wikiendi anaweza kuchinja mbuzi wanne mpaka mpaka sita na kuuza nyama yote.
‘’kwa siku za kawaida nachinja mbuzi watatu lakini inapofika siku za wikieni nachinja mbuzi watano mpaka sita na nauza nyama yote inaisha maana wateja wanakuwa wengi sehemu zote’’

Pichani ni Bw. Rafael Isaya akimuhudumia mteja

Aidha Bw John Paul ambaye pia nimfanya biashara wa nyama choma ameeleza changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ya wafanya biashara hao kuwa wengi sehemu hiyo na huku wengine wakiwa na wateja wao wa kudumu.

Amemalizia kwa kutoa ushauri kwa wafanya biashara wengine kufanya kazi hiyo katika hali ya usafi ili kuepuka mlipuko wa magonjwa ambayo ni hatari sana kwa binadamu.

Habari na ;OMARI SINGANO pamoja na GUDILA KULAYA

AJTC STARS NA AJTC QUEENS WAJIPANGA KUSHINDA BONANZA ARUSHA.

Pichani: kulia ni Mratibu wa michezo katika chuo cha uhandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw Onesmo Elia Mbise akizungumza na mwandishi wa habari Geofrey Mashauri kutoka Ajtc Tv.
 Timu kutoka chuo cha uhandishi wa habari na utangazaji Arusha{Ajtc stars &Ajtc queens}zimejipanga katika bonanza la vyuo vya ufundi mkoani Arusha.

Tuesday, 9 September 2014

UJASIRIAMALI NDIYO MKOMBOZI WA MWANAMKE NCHINI

Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha kwa kufanyakazi za ujasiriamali na kuacha kuwategemea wanaume zao katika kuendesha maisha.

Wito huo umetolewa na wanawake wauzao chakula (mama ntilie) jijini Arusha walipokuwa wanaongea na mwandishi wa habari hizi mapema leo.

              ‘’Inatakiwa wanawake tujishughulishe tuache kumtegemea mwanaume kwa kila kitu maana ajira zipo na hata wakija kwangu ninatoa ajira pia”,alisema mmoja wa wajasiriamali hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake

Pichani; Baadhi ya vyombo wanavyotumia wajasiriamali hao (picha na Nassor Amour)
Wakiongea kwa kusisitiza walisema wanawake wanatakiwa kujishughulisha Zaidi kwa kuwa wanaweza na si kila kitu katika kuendesha maisha wakamtegemea mwanaume tu.

Wanawake hao walielezea faida zinazopatikana ktokana na kazi za ujasiriamali kuwa ni kukidhi mahitaji yao ya kila siku,kupata umaarufu,kusaidizana majukumu na mwanaume na pia kujishughulisha kama mwanamke.

Aidha walibainisha changamoto wanazokutana nazo kutokana na kazi hizo za ujasiriamali kuwa ni wivu baina ya wao kwa wao,usumbufu na dharau kutoka kwa wateja na pia bwana afya kuwataka kuvalia sare wakati wa kazi

                   “Changamoto tunazokutana nazo ni wivu kwa sisi wenyewe,bwana afya analazimisha kuvaa sare,usumbufu kwa wateja na pia hawa wateja wetu hawatuheshimu kabisa”,aliongea Bi. Maryam Abubakar

Pichani; MMoja wa waateja wa wajasiriamali hao (Picha na Nassor Amour)
Pia walieleza kuwa kuna ushindani wanaopeana lakini wameeleza kuwa riziki anatoa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila dawa pekee ya ushindani huo ni kujituma na kuboresha huduma zao.

                   “Ushindani upo kila mahali ila kiukweli riziki inatoka kwa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila inatakiwa tuboreshe huduma zetu na kujituma pia”, alieleza mama Soni

Kwa upande wa wateja wao wamelaumu hali ya usafi katika mazingira wanayofanyia kazi na wakumbuke kuwa wanatoa huduma hiyo ya chakula kwa binaadamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wateja wa wajasiriamali hao Bi. Shadya Khamisi alisema huduma zao ni nzuri ila hakuna budi kupewa semina ya usafi.

Pichani; Bi.Shadya Khamisi akielezea hali ya usafi wa mama ntilie jijini Arusha(picha na Nassor Amour)
                     “Kiukweli huduma zao ni nzuri kiasi lakini usafi haupo unakuta mtu anapika kichwa kikiwa wazi na vumbi la magari na pikipiki linaingia kwenye vyakula ila ninaamini wakipewa semina ya usafi itakuwa vizuri zaidi”, alishauri Bi. Shadya Khamisi

Mwisho kabisa waliwaahidi wateja wao kuwa wategemee huduma bora zaidi kutoka kwao kqa vyakula bora na vyenye kujenga afya zao ila tu waheshimiwe kama watu wanaofanya kazi zingine.


Habari na Nassor Amour na Beatrice Mbowe


ARUSHA............ A.J.T.C:YABORESHA MIUNDOMBINU

   Afisa masoko wa chuo cha Uandishi uandi wa habari na  
                                utangazaji  Arusha  Israel Mungule Kulia,Akizungumza na Mwandishi wa habari                               Prisca Mushi  ofisini kwake mapema leo.picha na SALEHE ABDALLAH.

                       
Habari na Prisca Mushi,,Picha na SALEHE ABDALLAH.
Afisa masoko katika chuo cha uandishi wa habari  na utangazaji arusha bwana Israel mungure amebainisha mbinu mbalimbali wanazo tumia katika kukitangaza chuo hicho.

Akizungumuza  na waandishi wa habari mapema jana katika ofisa yake Bwana Mungure alisema kuwa wanatembelea shule mbalimbali za sekondari na kuwatangazia wanafuzi wanao hitimu kidato cha nne na kuwa na sifa za ufaulu ili kujiunga na  chuo hicho.

Aidha  alisema kuwa wanatumia vyombo mbalimbali vya habari kukitangaza chuo hicho kupitia  radio safina,sauti ya injili moshi,radio 5, na nyingine nyingi kupitia matangazo yanayorushwa kwa siku mara tatu.

Bwana; mungure  ameeleza pia kuwa wanatumia mitandao ya kijamii kama face book,tuvuti,pamoja na barua pepe ili kuhakikisha matangazo yao yanawafikia walengwa kwa wakati muafaka, 
‘Pia tunasambaza vipeperushi sehemu mbalimbali kwa ajili ya kukitangaza chuo chetu kwa watu ’’alisema mungure.

Pamoja na hayo mungure alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa  kupata wanafunzi wengi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro Tanga, Iinga Da es salaam pamoja na mikoa jirani ya Arusha.

     Alisema kuwa wanampango wa kuboresha  majengo na miundombinu  ili kupata wanafunzi wengi zaidi  kutoka sehemu mbalimba za nchi na pamoja na nje ya nchi.
Kutokana na uchache wa madarasa katika chuo hicho Mungure amesema wanampango wa utafuta eneo kubwa zaidi  ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote.

Sanjari na hayo  alibainisha changamoto wanazo kumbananazo ni pamoja na gharama za matangazo kuwa juu  kwa baadhi ya vyombo vya habari wanavyo vitumia katika kukitangaza chuo hicho
”Gharama za matangazo zipo juu na  kwawakati mwingine tangazo halipi gwi kwa wakati kama mkataba unavyo sema”alisema israei mungure.

 Alimalizia kwa kuwashauri wazazi   na walezi  kuwaleta watoto wao ili kupata elimu bora ya uandishi wa habari na utangazaji kwani ni chuo  hicho kina shikilia nafasi ya  pili kwa  ubora hapa nchini kutokana na kuwa  na walimu  bora studio za Radio na Tv za mafunzo kwa vitendo  ili kuwa patia uzoefu wanafunzi wanao soma katika chuo hicho.










UJASIRIAMALI NDIYO MKOMBOZI WA MWANAMKE NCHINI



 Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha kwa kufanyakazi za ujasiriamali na kuacha kuwategemea wanaume zao katika kuendesha maisha.

Wito huo umetolewa na wanawake wauzao chakula (mama ntilie) jijini Arusha walipokuwa wanaongea na mwandishi wa habari hizi mapema leo.

Baadhi ya vyombo vinavyotumiwa na wajasiriamali hao(picha na Nassor Amour)
  
              ‘’Inatakiwa wanawake tujishughulishe tuache kumtegemea mwanaume kwa kila kitu maana ajira zipo na hata wakija kwangu ninatoa ajira pia”,alisema mmoja wa wajasiriamali hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake

Wakiongea kwa kusisitiza walisema wanawake wanatakiwa kujishughulisha Zaidi kwa kuwa wanaweza na si kila kitu katika kuendesha maisha wakamtegemea mwanaume tu.
Wanawake hao walielezea faida zinazopatikana ktokana na kazi za ujasiriamali kuwa ni kukidhi mahitaji yao ya kila siku,kupata umaarufu,kusaidizana majukumu na mwanaume na pia kujishughulisha kama mwanamke.

Aidha walibainisha changamoto wanazokutana nazo kutokana na kazi hizo za ujasiriamali kuwa ni wivu baina ya wao kwa wao,usumbufu na dharau kutoka kwa wateja na pia bwana afya kuwataka kuvalia sare wakati wa kazi

                   “Changamoto tunazokutana nazo ni wivu kwa sisi wenyewe,bwana afya analazimisha kuvaa sare,usumbufu kwa wateja na pia hawa wateja wetu hawatuheshimu kabisa”,aliongea Bi. Maryam Abubakar
  
Pia walieleza kuwa kuna ushindani wanaopeana lakini wameeleza kuwa riziki anatoa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila dawa pekee ya ushindani huo ni kujituma na kuboresha huduma zao.

                   “Ushindani upo kila mahali ila kiukweli riziki inatoka kwa mungu na kila mmoja ana fungu lake ila inatakiwa tuboreshe huduma zetu na kujituma pia”, alieleza mama Soni

Kwa upande wa wateja wao wamelaumu hali ya usafi katika mazingira wanayofanyia kazi na wakumbuke kuwa wanatoa huduma hiyo ya chakula kwa binaadamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wateja wa wajasiriamali hao Bi. Shadya Khamisi alisema huduma zao ni nzuri ila hakuna budi kupewa semina ya usafi.

                     “Kiukweli huduma zao ni nzuri kiasi lakini usafi haupo unakuta mtu anapika kichwa kikiwa wazi na vumbi la magari na pikipiki linaingia kwenye vyakula ila ninaamini wakipewa semina ya usafi itakuwa vizuri zaidi”, alishauri Bi. Shadya Khamisi

Mwisho kabisa waliwaahidi wateja wao kuwa wategemee huduma bora zaidi kutoka kwao kwa vyakula bora na vyenye kujenga afya zao ila tu waheshimiwe kama watu wanaofanya kazi zingine.

Habari na Nassor Amour na Beatrice Mbowe 

Sunday, 7 September 2014

Alshabaab lathibitisha kifo cha Godane


NA SALEHE ABDALAH,,,,,CHANZO BBC SWAHILI
Wapiganaji wa Alshabaab

Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.

Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu .
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo hafahamiki vyema.