Wednesday, 2 July 2014

TAIFA STARS WALALA UGENINI





 Na Mercy Rodricky
WENYEJI Botswana Leo hii huko Uwanja wa Taifa Jijini Gaborone wameichapa Tanzania Bao 4-2 katika Mechi ya Kirafiki. 


Taifa Stars ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Mcha Khamisi kufuatia Difensi ya Botswana kujichanganya lakini Timu hiyo, inayoitwa Zebras, ilisawazisha kabla Mapumziko kwa Bao la Kichwa la Jerome Ramatlhatwane.

Hadi Mapumziko, Zebras 1 Taifa Stars 1.
Kipidi cha Pili, Zebras walikuja moto na kupiga Bao 3 kupitia Lemponye Tshireltso, Bonolo Phuduhudu na Kijana wa Miaka 19, Karabo Phiri.

Taifa Stars walifunga Bao lao la Pili kwa Penati ya Dakika ya 76 ya John Bocco.
Mechi hii ilikuwa ya kujipima nguvu kwa Timu zote mbili kwa ajili ya Mechi za Mchujo za AFCON 2015 ambapo Taifa Stars wataivaa Msumbiji Jijini Dar es Salaam hapo Julai 20 na Zebras kucheza na Guinea Bissau Julai 19.

Taifa Stars, ambao wako chini ya Kocha Mart Nooij, waliwasili huko Gaborone kwa Kambi ya Mazoezi tangu Juni 24 na wamekuwa wakifanya Mazoezi Uwanja wa SSKB wakiwa na Kikosi kamili kasoro Wachezaji wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Jumamosi, huko huko Gaborone, Taifa Stars watajipima nguvu na Lesotho.

No comments:

Post a Comment