Wednesday, 2 July 2014

WAUAJI WA MTAWA DAR WAKAMATWA

 www.ajtctv@gmail.com
habari na
HADIJA HASSAN
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi ambao wanahusishwa na mauaji ya mtawa wa
kanisa Katoliki Sista Clezensia Kapuli,mbali na watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashikiliwa wakihusishwa na matukio mbali mbali ya ujambazi nchini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar esSalaam Kamishna Suleiman Kova amewataja majambazi wanaohusishwa na mauaji ya Sista Kapuli kuwa ni Manase Ogenyeke “mjeshi” (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe na Hamis Shaban “Carlos” mkazi wa Magomeni mwembechai.
Wengine waliokamatwa kutokana na matukio ya ujambazi ni Beda Mallya miaka (37) mkazi wa Mbezi msakuzi, Michael Mushi (50), Sadick Kisia (32), Elibariki Makumba (30), Nurdini Suleiman (40) pamoja na Mrumi Salehe (38).

Majambazi hao wamekamatwa kutokana na oparesheni inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha mtawa huyo aliyefariki dunia mnamo Juni 23 mwaka huu,kamanda Kova amesema majambazi hao wawili licha ya kuhusishwa na tukio la kifo cha mtawa huyo, pia wanahusika na tukio la uporaji fedha katika benki ya Barcrays tawi la Kinondoni lililotokea miezi michache iliyopita.

No comments:

Post a Comment