Thursday, 3 July 2014

TANZANIA YATWAA TUZO

 
Dar es Salaam. Tanzania inaongoza kwa kuwa na mitaji mikubwa ya uwekezaji kutoka nje katika nchi za Afrika Mashariki, ripoti mpya imebainisha.
Kwa mujibu ripoti hiyo ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ya mwaka 2013, Tanzania ina mitaji kutoka nje yenye thamani ya Dola 12.7 bilioni za Kimarekani.
Tayati Tanzania imezipita nchi ya Kenya yenye Dola 3.4 bilioni na Uganda Dola 8.8 bilioni.
Katika mwaka 2013 pekee, Tanzania ilivutia mitaji ya uwekezaji kutoka nje yenye thamani ya Dola 1.9 bilioni za Kimarekani na kuiacha mbali Kenya iliyovutia Dola 514 milioni za Kimarekani.
Na Linah Mvungi

No comments:

Post a Comment