Wafanya biashara katika soko la Mbauda mkoani Arusha
wameulalamikia uongozi wa kata ya sombetini lilipo soko hilo juu ya uchafu
unaoletwa na wakazi wa jirani na soko hilo.
Akizungumza
na muandishi wa habari hizi mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Mikaeli Materu
amesema kuwa uchafu wa soko hilo unachangiwa na majirani wa soko hilo kuleta
takataka kutoka majumbani mwao.
Bwana
Mikaeli Materu akitoa maelezo wakati akizungumza na muandishi wa habari sokoni hapo . Picha na Rosemery Mmbando.
Bwana Materu
ambaye ni mfanya biashara wa sokoni hapo tangu miaka ya 1990 amesema uchafu
kama nywele na ngozi za wanyama ni uchafu usiozalishwa sokoni hapo lakini
utaukuta katika mazingira ya soko hilo.
Akibainisha
changamoto nyingingine bwana Materu amesema ukosefu wa mtaro wa maji taka
sokoni hapo ni kero ambayo inawasumbua na hujitokeza zaidi katika kipindi cha
mvua.
Pamoja na
kuwa na kero hizo Bwana Materu amesema licha ya wenyeji na uzoefu alionao
sokoni hapo hatambui kama kuna uongozi wa soko au lah.
Mpangilio
mbovu wa wafanya biashara na mazingira machafu katika soko la mbauda mkoani
Arusha. Picha na Rosemery Mmbando.
Juhudi za
kumpata diwani wa kata ya sombetini Bwana Ally Bananga hazikufanikiwa kutokana
na kutokuwepo katika ofisi ya kata hiyo.Bwana Materu
alimaliza kwa kuuomba uongozi wa kata hiyo na halmashauri kuboresha mazingira
ya soko ili kupunguza msongamano wa wafanya biashara katikati ya jiji la
Arusha.
Biashara zikiendelea sokoni hapo bila ya kujali hali ya usafi
wa mazingira yenyewe.
Picha na Rosemery Mmbando.
Soko la Mbauda
katika kata ya Sombetini mkoani Arusha si soko rasmi lakini hata hivyo limekua
msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.
Habari na; Eliamini Mchome na Rosemery Mmbando.